Loading...

Ukweli kuhusu taarifa za Mbwana Samatta kuhamia AS Roma ya Italia

Good news kwa watanzania wote kwa mwaka 2016 ilikuwa ni headlines za nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta kujiunga na KRC Genk yaUbelgiji, lakini leo July 5 2016 jina la Samatta limerudi tena kwenye headlines za usajili.
Kuanzia usiku wa July 4 hadi leo July 5 habari zilizokuwa zimesambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu Samatta ni kuwa yupo njiani kujiunga na klabu ya AS Roma ya Italia, hii ni taarifa ambayo imeenea kwa kiasi kikubwa hata kufikia baadhi ya wanasoka Tanzaniakutumia social network zao  kumpongeza.
sama 1
Mchezaji wa Yanga Haruna Niyonzima
Baada ya habari hii kuenea kwa kiasi kikubwa, millardayo.com ilimpata meneja wa staa huyo Jamal Kisongo atueleze ukweli wa taarifa hizo “Huo ni uzushi tu hata sijui umetoka wapi na mimi nimesikia mitandaoni, lakini nimewasiliana na Samatta hakuna habari kama hizo wala mawakala wake hawana taarifa hizo”
sama 2
Baadae katika Amplifaya ya Clouds FM umtamsikia Kisongo akielezea zaidi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright CHACHANDU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top