Loading...

JACK Wolper Adaiwa Kunasa Mimba!

Habari ya mjini! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe, anadaiwa kunasa ujauzito wa mwandani wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ hivyo yupo mbioni kutimiza ndoto yake ya kupata mtoto hivi karibuni.

Habari za uhakika kutoka kwa watu wa karibu wa mastaa hao zilidai kwamba, ishu hiyo ni mpango wa wasanii hao kwa kuwa walipanga mwanzoni wakati wa kuanzisha uhusiano wao hivyo kwa tukio hilo kila mmoja ana furaha na wamejipanga kumpokea mgeni wao.
Chanzo hicho kilimwaga ubuyu kwamba, hivi karibuni, Wolper na Harmonize waliingia kwenye mgogoro kidogo lakini lilipoibuka suala la mrembo huyo kunasa ujauzito, ndipo uhai wa penzi lao ukarejea kwa kiwango cha juu.

“Ni kweli hapo nyuma walizinguana lakini baada ya mimba, sasa hivi penzi lao lipo kwenye ubora wake na kila mmoja anafurahia jambo hilo kwa sababu wamejipanga,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Wikienda lilimsaka Wolper ili kuthibitisha madai hayo ambapo alisema kuwa kama tulivyoipata habari hiyo, kama ni kweli hakuna tatizo lolote yeye kupata ujauzito.
“Jamani habari nyingine ni njema sana, kama kuna mtu amewaambia basi siyo mbaya maana nipo huru kuwa mjamzito kwani sijasababisha chochote kibaya kwa mtu,” alisema Wolper huku Harmonize akisisitiza kuwa Wolper ndiye msemaji pekee wa suala hilo.
GPL

SHUHUDIA Warembo Wajiachia na Ben Pol Red Carpet Basement

MAISHA CLUB (17)
Mrembo ambaye ni mwanamitindo Hamisa Mobeto akiwa na mkali wa Bongo Fleva, Ben Pol usiku wa kuamkia leo Maisha Basement katika usiku wa Moyo Mashine.
MAISHA CLUB (18)MAISHA CLUB (19)
MAISHA CLUB (20)
MAISHA CLUB (14)
Mashabiki wakiendelea kujiselfisha na mastaa hao.
MAISHA CLUB (4)MAISHA CLUB (5)
MAISHA CLUB (1)

Aibu 20 za Wanaume Endapo Mwanaume Atafanya Haya Kwenye Mahusiano ya Mapenzi


AIBU 20 ZA WANAUME:

1. Japo maisha ni kusaidiana ni aibu na fedheha mwanaume kulishwa na mkewe.🙈

2. Ni aibu na fedheha mwanaume kuhamia kwenye nyumba ya mkeo ukakala ukakoroma na taulo ukafunga..🙈

3. Ni aibu na fedheha kuendesha gari la mkeo wakati wewe hujawahi kumiliki gari alafu unawaka wivu juu yake.🙈

4. Ni aibu na fedheha kuishi na mwanamke ambaye wakwe zako wanajua kuwa anakuzidi uwezo.🙈

5. Ni aibu na fedheha kumuoa mwanamke ambaye anamiliki uchumi wa familia hata watoto anasomesha yeye wewe unajivunia urefu wa kimo🙈

6. Ni aibu na fedheha kila likizo unaenda kijijini kwa mkeo na watoto wote kisa yeye anazohela🙈

7. Ni aibu na fedheha kukaa miaka mingi unamlaumu mkeo kuwa hazai wakati wewe huna hata mtoto wa kusingiziwa🙈

8. Ni aibu na fedheha kumrudia mwanamke aliye kuacha yeye mwenyewe kipindi kirefu na akaamua kukurudia yeye mwenyewe tena kwa masharti kutoka kwake.🙈

9. Ni aibu na fedheha kupewa zawadi ya kiwanja na wakwe zako siku ya send off.🙈

10. Ni aibu na fedheha kujenga kwenye kiwanja cha mkeo wakati wewe hujawahi kumiliki kiwanja🙈

11. Ni aibu na fedheha kulelewa mtoto wako na baba wa kambo wakati wewe upo unaishi na unajiita kidume🙈

12. Ni aibu na fedheha kukaa kwenye nyumba yenye fenicha zoote kanunua mkeo🙈

13. Ni aibu na fedheha kusimamia ujenzi wa nyumba ya mkeo wakati wewe huchangii hata shilingi mia🙈

14. Ni aibu na fedheha kulea mtoto ambaye sio wa kwako kwa kisingizio cha kitanda hakizai haramu wakati mkeo anajua mtoto yule sio wa kwako.🙈

15. Ni aibu na fedheha kulala kimapenzi na mwanamke ambaye anajua kuwa wewe unajua na unaushahidi wa michepuko yake🙈

16. Ni aibu na fedheha kumbembeleza mwanamke anayejua kuwa anakukosea kwa makusudi🙈

17. Ni aibu na fedheha kumaliza makanisa ukiwahadithia wachungaji tabia mbaya na usaliti wa mkeo🙈

18. Ni aibu na fedheha mkeo kukunyima unyumba ukaenda kumshitaki kwa wazazi wake wakati unajua cha kufanya🙈

19. Ni aibu na fedheha mara kukopakopa kwa wakwe zako tena waliostaafu kazi..ni aibu ni aibu kubwa.🙈

20. Ni aibuu na fedheha kwenda baa na mke baa au sehemu za starehe kila siku ikija bili unapewa wewe nawe unampa mkeo alipe kazi kukuna tu kidevu na kwenye wallet umejaza business card na viwembe vya kugushi nyaraka mitaani🙈

Hizo ni baadhi tu ya aibu za wanaume waliowengi karne ya leo. Sambaza kwenye ma group wajijue na wamuombe Mungu awafungulie milango nao wawe wanaume katika nyumba zao

‎Diamond‬ Platnumz Kikaangoni Tena na ‪‎Skendo‬ ya ‪Kujiweka‬ Kimapenzi kwa ‪Hamisa‬ Mobetto

‎Baada‬ ya Kumaliza Skendo ya ‪‎Kutoka‬ Kimapenzi na ‪Video‬ queen wa Kwetu ya Raymond, ‪‎Diamond‬ Platnumz Kikaangoni Tena na ‪‎Skendo‬ ya ‪Kujiweka‬ kwa ‪Hamisa‬ Mobetto

Tetesi hizo za Hamisa Kutoka na Diamond zimepigiliwa msumari kwa kitendo cha juzi kwenye birthday ya Mama yake Diamond ambapo Hamisa alionekana kuwa karibu zaidi na familia ya Diamond hasa Mama na Dada yake Dai Asma Platnumz, Kitendo hicho kilitafsiriwa na wengi kuwa ndio chombo kipya cha Diamond hasa ukichukuliwa kuwa inasemekana familia hiyo ya Diamond kwa sasa haziivi na Zari ambae ndio mpenzi wa Diamond kwa sasa...

Nilivyofanya Bonge la Sherehe Baada ya Mke Wangu Kufukuzwa Kazi

Huyu mke nilimuoa akiwa hana kitu, kwa bahati alitafutiwa kazi na ndugu yake kwenye kampuni moja ya simu akawa analipwa kama milioni 3 kwa mwezi fasheni na yeye yeye na fasheni vipodozi kila aina,handbag na nywele za laki mbili ndio mshahara wake ukawa unaishia huko mimi mshahara wangu hauzidi laki sita,nilifanyishwa vituko vyote ndani ya nyumba ,manyanyaso yote ,hapiki hafui,hafanyi chochote ndoa ikawa inaelekea kuvunjika.

Nikaenda mahakamani kuprocess talaka wakasema mpaka nianzie baraza la usuluhishi la kata au kanisani,nikaamua kwenda kanisa tulilofungia ndoa tukaitwa kwa Baba Paroko for hearing sijui mediation sijui arbitration sijui mie nikatinga kwa bajaj ya kukodi nimepaukaaa yeye akaja na RAV4 .
Baba Paroko alivyotusikiliza akaaniita pembeni akasema kijana hapa nadhani hata tukiomba na kukariri mistari yote ya biblia plus mapambio yote ndoa yako haitarudi kama mwanzo pambana utafute hela ,huyu ni mchaga katumwa pesa mjini

Nilisali sana nikasugua goti nikamuomba Mungu mara mambo yangu yakakaa sawa mshahara ukawa mara mbili plus marupurupu anagalau . baada ya miezi miwili sina hili wala lile mara simu yangu nilishangaa mke wangu kunipigia mchana ,tumeachishwa kazi kmpuni imeuzwa,hureeeeee niliruka ruka kwa furaha sana nikapigia simu washikaji tukaenda kunywa bia na nyama choma mpaka saa sita usiku kabla polisi na makonda hawajatuvamia nilijua ile kazi ndio inaniharibia ndoa na aliipata kibahati hawezi tena kupata kazi kama ile.

Hela yote ya NSSF akajaribu kufanya kila biashara biashara zikabuma mtaji ukakata alijifanya hajui kupika sasa anapika kuliko hata wapishi wa Kempinski,alijifanya sijui hawezi kufua sasa anafua kuliko dobi ,kitandani alijifanya mvivu sasa yuko vizuri kuliko wacheza shoo wa fally ipupa ,RAV4 imepaki tu muda wote ananilelea watoto kwa nini nisimshukuru Mungu

Funzo:
Wanawake Msijisahau sana pale mnapokuwa vizuri kifedha zaidi ya mume
Older Posts
© Copyright CHACHANDU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top