Mchezo wa kwanza uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Serengeti ilishinda mabao 3-0.
Katika mchezo wa jana, Serengeti iliandika bao la kwanza katika dakika ya tisa lililofungwa na Ibrahim Abdallah kabla ya Mohamed Abdallah aliifungia Serengeti bao la pili kwa shuti kali dakika ya 43.
Asad Juma alifunga bao la tatu dakika ya 50 na Issa Makamba alifunga bao la nne kwa mkwaju wa penalti dakika ya 61 baada ya kufanyika madhambi eneo la adhabu.
Asad aliifungia Serengeti bao la tano dakika ya 70 baada ya kuwatoka mabeki wa Shelisheli na Yohana Mkomola alihitimisha kwa kufunga bao la sita dakika ya 90.
Post a Comment