Lugola, Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Lupa na Murad Sadiq, Mbunge wa Mvomero wanatuhumiwa kuomba rushwa ya Sh. 30 mil kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Gairo tarehe 15 Machi mwaka huu.Lugola ametoa madai hayo leo mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo baada ya wakili wa seriksli Denis Lekayo kueleza kuwa, waendesha mashtaka wa kesi hiyo hawapo.
Wakili Lekayo amedai kuwa, shauri hilo liliitishwa kwa ajili maelezo ya awali lakini waendesha mashtaka hawakupo.
Kutoka na maelezo hayo Lugola amedai kuwa, ikemee tabia hiyo ya kuahirishwa kesi mara kwa mara.
Lugola amedai kuwa, kitendo hicho kinawanyima haki yao ya msingi ya kufanya shughuli zao za Bunge.
Imekuwa kawaida kwa washtakiwa wanapokuwa watoro mahakama huwaita kuthibitisha kwa nini wakeshindwa kuhudhuria.
Baada ya kueleza hayo, Lekayo ameiomba mahakama radhi na kusema ‘tutafanya haraka kesi iendelee.’
Hakimu Simba amesema, kauli iliyotolea na mshitakiwa ni ya msingi. Baada ya kueleza hayo ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 12 Julai mwaka huu kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
Post a Comment