Waziri
Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim amesema wanajeshi 2,839 wakiwemo
maafisa wa ngazi za juu, wamekamatwa baada ya jaribio la mapinduzi
lililozimwa.
Miongoni
mwa wanaoshikiliwa wamo majenerali wawilia wa jeshi, kwa mujibu wa
vyombo vya habari vya nchi hiyo.
Waziri
Mkuu huyo ameliita jaribio hilo la mapinduzi kama doa jeusi katika
demokrasia, na kueleza kuwa raia 161 wameuwawa na wengine 1,440
wamejeruhiwa.
Raia wenye hasira wakiwadunda wanajeshi baada ya kuwadhibiti na kuzima jaribio lao la mapinduzi
Mwanajeshi aliyedhibitiwa na raia akipigwa ngumi nzito ya shavuni na mmoja wa raia
Post a Comment