Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwingulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alipokua akizungumza na maofisa wakaguzi wa Jeshi la Polisi pamoja na askari wa vyeo mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma.Amesema, tatizo la makazi kwa askali wa Jeshi la Polisi ni changamoto kubwa inayotakiwa kutatuliwa kwa haraka ili kuwafanya askari kuwa na moyo wa kufanya kazi ya kulinda raia na mali zao kwa kuzuia uhalifu.
“Tutahakikisha tunatengeneza makazi rafiki wa askali wetu ili waweze kuchapa kazi kwa kwa ufanisi zaidi na kupambana na wahalifu wa aina yoyote, ”amesema Nchemba.
Amesema, kutokana na tatizo hilo serikali itatumia njia mbadala ya kuhakikisha linatatua tatizo la makazi kwa jeshi la polisi kama sio kulimaliza kabisa .
Aidha ametoa rai kwa askali hao kuzingatia miiko yao ya kazi na wanapofanya kazi kama walivyofundishwa vyuoni na kuapa pindi walipoingia kazini.
“Endapo mtazingatia miiko ya kazi yenu haitatokea siku ambayo nitakuwa na mashaka na utendaji kazi wa jeshi la polisi.
“Muhakikishe mnatenda haki kwa kila mtu na msiwe na tabia ya kuwakandamizi wanyonge kama baadhi ya askali wengine wanavyofanya,nyie mnatakiwa kuhakisha mnawatetea wanyonge kuweza kupata haki zao za msingi,”amesema Nchemba.
Pia amewataka kutumia nguvu kubwa katika kuhakisha wanalinda usalama wa nchi na raia ili kuwafanya wananchi kuwa na imani na jeshi la polisi.
Hata hivyo amesema serikali ya amwamu ya tano inamikakati ya kuboresha maslahi ya askali wote .
Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma amesema, hana shaka na askali wake kwani wanachapa kazi usiku na mchana kwa kuzingatia maagizo kutoka makao makuu na anyotoa yeye.
“ Tunafanya kazi kwa weredi kuhakikisha nchi inakuwa shwari kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi,” amesema kamanda Mambosasa.
Post a Comment