Na Isack (Babati, Manyara)
Nianze kwa kuipongeza timu ya Yanga kwa hatua waliyofika kwenye michuano
ya kimataifa (robo fainali) ni hatua kubwa, pongezi hizi ziwafikie
viongozi, wachezaji, wanachama, mashabiki na watanzania wote kwa
ujumla, Yanga inawakilisha Tanzania na ikifanya vizuri Tanzania itakuwa
imefanya vizuri, isipofanya vizuri itakuwa Tanzania haijafanya vizuri.
Baada ya utangulizi huo, ninavitu vichache ambavyo nafikiri vitaisaidia timu ya Yanga kutoka ‘wakimataifa’ hadi timu tajiri.
Mpira wa miguu ni biashara inayolipa kupita biashara zote ambazo ni halali hapa duniani kwa sasa. Ni kwa ufahamu wangu mdogo.
Nasema Yanga kutoka wa kimataifa hadi timu tajiri kwa sababu zifuatazo:-
Yanga inamashabiki wengi hapa nchini kuliko timu yeyote ikifuatiwa na
Simba kulingana na maeneo mbalimbali ambayo nimeishi hapa Tanzania japo
wengine watanibishia. Sipo hapa kwa ajili ya kubishana ila natoa mawazo
yangu tu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji pato la Yanga kwa mwaka
ni billion 1.5, lakini matumizi ni bilioni 4, bilioni 2.5 anatoa mfukoni
kwake.
Kwa mawazo yangu Yanga ni timu tajiri sana kama nitakavyoeleza hapa chini:-
Yanga inamashabiki zaidi ya milioni 10, lakini wanachama sidhani kama
wanazidi milioni 2. Ok ni assume wanachama hai ni laki 3 nchi nzima na
watakao kuwa hai (kulipia kadi) kwa muda wa miaka 5 ijayo ni 135,100 tu
hapa yanga inauwezo wa kupata billion 14.1 (14,100,000,000) kwa mwaka
kwa sababu zifuatazo.
NA | AINA WA UANACHAMA | IDADI | ADA | ADA KWA MWEZI | ADA KWA MWAKA |
1 | Wanachama wa kawaida. | 100,000 | 2,500 | 250,000,000 | 3,000,000,000 |
2 | Wanachama wa kati | 30,000 | 10,000 | 300,000,000 | 3,600,000,000 |
3 | Wanachama (VIP) | 5,000 | 100,000 | 500,000,000 | 6,000,000,000 |
4 | Wanachama wa heshima. | 100 | Hawa hawalipi ni kama Mama Fatuma Karume wengine | ||
Jumla ndogo | 12,600,000,000 |
Kwa mawazo yangu Yanga inatakiwa kuwa na aina nne za wanachama kama ilivyo kwenye hili jedwali hapa chini.
Ukijumlisha na billion 1.5 kwa maelezo ya Mwenyekiti ambazo zinapatikana kwa mwaka, jumla kuu ni 14,100,000,000.
Na hii inawezekana kabisa, leo hii haiwezakani mwanachama analipa elfu
12 kwa mwaka anakuwa na sauti kwenye timu hii ni ajabu. Wakati
wanapendekeza kiwango cha elfu 1 kwa mwezi nadhani dollar moja ilikuwa
sawa shilingi elfu 1, leo hii dollar 1 ni sawa na shilingi elfu 2,200
(wastani).
Nimeweka magroup manne ya wanachama ili kutoa hamasa watu wajitoe (wachangie) na kutambua umuhimu wao.
Mfano group na 1 hakuna haja ya kupiga kura, kura wapige kuanzia group
no 2. Nina sababu mtu amechangia elfu 30 kwa mwaka na wakati kukodi
ukumbi, kuchapisha karatasi za kupigia kura, chakula, ulizi, posho za
wasimamizi n.k kwa siku ya kupiga kura ni gharama kubwa sana (mimi
nitakuwa kwenye hili group no 1). Wanachama kundi la 3 ni wale marafiki
kama Ndama mtoto ya Ng’ombe, David Mosha, Jerry Muro, Wema Sepetu,
Waheshimiwa wabunge n.k. kundi la nne ni watu mwenye michango ya muda
mrefu kama Mh. Magufuli, Mh. Jakaya Kikwete, Mama Fatuma Karume, Yusuph
Manji na wengine ambao siwajui.
Hata uwanjani kuna madaraja mbalimbali, VIP C na B, VIP A iwe kwenye
ndege n.k na hii itaongeza hamasa kwa wanachama kutoka daraja moja
kwenda jingine.
Kuwa na database ya wanachama ambapo mwanachama asipo lipia computer
(system) ina mwalert na asipolipa miezi 3 system inamtoa na inabidi
aombe umpya au kulipa fine.
Timu itaweza kuingiza billion 14.1 au zaidi kwa mwaka?
Matumizi ya club
Matumizi ya club kwa mwaka kwa mujibu wa Mwenyeki ni billion 4 tu, na
ongeza billion 1 iwe billion 5 kwa mwaka. Club itabaki na billion 9.1
ambazo ni fedha nyingi sana zinaweza kufanya yafuatayo kwa mwaka mmoja.
- Club inawezaka kununua maeneo kwenye kanda zote 4 (Kaskazini, Kanda ya ziwa, Kati na Kusini) Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya.
- Maeneo ya pembezoni mikoani siyo ghali kama Dar es salaam, club itaweza kuwa na vitega uchumi vya kutosha. Ekari moja mikoani ni wastani wa million 10 x 10 ekari = 100,000,000 kanda zote 4 sawa na million 400,000,000 chenji inabaki billion 8.7 ambayo itatumika kujenga uwanja ambao hauzidi billion 2, kwa viwanja 2 ni sawa na billion 4. Hostels, guest houses nzuri na sehemu za wazi kwa ajili ya sherehe (beach/garden) 2@ billion 2 (Arusha na Mwanza)= 4 billion Hapo ni mwaka wa kwanza, mwaka unaofuata ni Dodoma na Mbeya kwa wastani wa billion 4 @ (uwanja, hostel, quest house/hotel, beach/garden).
- Mikoani quest/hotel ya billion 2 ni ya kisasa hapo pamoja na ukumbi, swimming pool, garden, sehemu za kufanyia michezo n.k
- Kujenga uwanja Dar es salaam hapa ni mwaka wa tatu na wa nne. Billion 9.1 zinatosha kuanza ujenzi uwanja wa kisasa pembeni mwa jiji ambapo mnaweza kununua ekari 10 @ million 40,000,000 = 400,000,000. Billion 8.7 ikatumika kwa ajili ya ujenzi, kwa miaka 2 billioni 16 ni uwanja wa kisasa.
FAIDA
- Club itakuwa ikisafiri kwenda mikoani inafikia kwenye maeneo yake hakuna gharama za uwanja wa mazoezi, kulala na chakula.
- Timu ya vijana (Academy) itatumia kituo kimoja kama kambi yake.
- Fedha za kuendeshea Academy zitapatikana kutokana na vitega uchumi hivyo.
- Kumbi zitakodishwa, guest wageni mbalimbali watafikia, timu mbalimbali zitakodi uwanja pamoja na hostel.
- Timu itaongeza ajira kwa wanachama wake kwenye kanda (mfano; Meneja, Mhasibu, ICT Officer, Dereva, Wahudumu, Walizi na Wapishi n.k).
- Timu inaweza kukopa mkopo mkubwa toka bank kama CRDB, TIB n.k kupitia asset zake.
- Timu itakuwa inachagua iweke wapi kambi kwenye sehemu tulivu.
- Timu itajitengemea daima bila kumtegemea mtu/mwanachama yeyote.
- Timu itakuwa karibu na wanachama wake wa mikoani ambapo wataweza kuteua wenzao wa kuwawakilisha kwenye mkutano mkuu.
- Timu itavutia wafadhili wengi zaidi
- Timu itavutia wawekezaji wengi wa ndani na nje.
- Timu itakuwa na uwezo wa kusajili wachezaji wazuri zaidi.
- Timu itavutia wachezaji wazuri kutokana na mazingira mazuri.
- Timu itakuwa na uchumi imara na Manji hataongezea billion 2.5 kwa mwaka.
- Timu itachangia pato la taifa kwa kulipa kodi, ajira n.k
- Billion 2.5 anazotoa Manji zitawasaidia wananchi wa kata ya Mbagala, kwa miaka 5 Mbagala itakuwa kama Ulaya.
- Timu itakuwa na uwezo wa kuingiza kipato cha milioni 50 kwa mwezi kwa kila kanda, kanda 4 sawa na million 200 na kwa mwaka billion 2.4 nje na wanachama.
Hizo ni baadhi ya faida ambazo inaweza kuzipata kwa mawazo yangu.
Faida zipo nyingi sana lakini sitaweza kuzitaja zote, hizo ni baadhi tu.
Hitimisho
Timu ianjiri Marketing Officer kazi yake aitangaze na kuishauri vizuri
timu ili kuuza bidhaa (products) mbalimbali, ICT Officer kwa ajili ya
ku-update website ambapo itatumika ku-update taarifa mbalimbali kama
(historia ya timu, majina ya viongozi, wachezaji, vikombe n.k) na kuwa
timu ya kisasa, watu watatumia kutangazia biashara zao.
Kwa kuanzia mtaji mnaweza kukopa bank CRDB, TIB n,k hata billion 2 tu
baada ya kuandika proposal/andiko nzuri ambapo mtaweza kuzishawishi
bank. Naamini wanachama wakihamasishwa vizuri wanaweza kuzilipa kupitia
michango yao bila tatizo.
Baada ya miaka mitano Yanga itakuwa mbali sana hapa Afrika.
Mkiyafanya haya Yanga mtakuwa timu Tajiri badala ya ‘wakimataifa’ na
inawezekana baada ya miaka 5-8 mtakuwa na ndege yenu na kuwa club ya
kwanza Tanzania kuwa ndege.
Yote yawezekana pale mtakapokuwa na mpango mkakati wa muda fupi, kati na mrefu.
Nawatakia mafanikio mema.
0715163816
Babati – Manyara.
Nakala
Wadau wa michezo wote Tanzania.
Post a Comment