“TAIFA linapita katika kipindi kigumu, ni wakati sasa watu tukaungana kutetea taifa letu. Tusipofanya hivyo wengi wataumizwa.
“Tuna kila sababu ya kuzuia hali hii mwanzo ili tufike salama, kila mpenda demokrasia ni wakati sasa wa kuungana na kuhakikisha demokrasia inaheshimika nchi.”Ni kauli ya Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki iliyopenyezwa nje jana usiku na mjumbe mmoja baada ya kukataliwa kupewa dhamana kutokana na kudaia kutoa kauli tata dhidi ya serikali..
Lissu ambaye ni Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana alilazwa rumande katika Kituo Kikuu ca Polisi, Dar es Salaam.
Muda wowote kuanzia sasa kiongozi huyo ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Makazi Kisutu kujibu tuhuma za kutoa kauli za uchochezi.
Tuhuma hizo zinakuja ikiwa ni siku bili tu tangu mbunge huyo kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za uchochezi ambapo gazeti la Mawio lilinukuu taarifa yake kuwa, uchaguzi wa Zanzibar ungesababisha machafuko.
Msingi wa tuhuma za Lissu jana ni kuwa, baada ya kusikiliza shauri lake la uchochezi Mahakamani Kisutu, ndani ya mahakama hiyo alizungumza na waaandishi wa habari kuwa tuhuma zake hazina msingo wowote.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi liligoma kueleza sababu za kukamatwa kwa Lissu na kuhojiwa pia kunyimwa dhamana.
Hata hivyo, John Malya, mwanasheria aliyeongozana na Lissu alisema, sababu kuu ni kauli yake ya ‘dikteta uchwara.’
Nje ya Mahakama ya Kisutu Jumanne wiki hii Lissue alisema, vitendo vinavyofanywa na serikali ya sasa ni vya hovyo.
“Kila msema kweli wa nchi hii. Huu ni wakati wa kujitokeza na kusema hii ni nchi ya vyama vingi, hii ni nchi inayotambua haki za binadamu kwenye Katiba yake.
“Hatuwezi tukakubali nchi iongozwe kwa kauli za mdomo za mtu mmoja hata kama amechaguliwa kuwa rais,”
Alipozungumzia kesi iliyofunguliwa na kuhusishwa kwake Lissu amesema, kesi iliyofunguliwa na serikali dhidi yake na wahariri wa gazeti la Mawio ya uchochezi, ni ushahidi tosha kuwa nchi imeingia kwenye giza nene la udekikteta.
Alisema, hata sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ipo wazi kwamba, kuikosoa serikali sio uchochezi.
“Mashtaka haya yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezo, sio ya uchochezi hata kidogo. Nilichosema, niliulizwa na waandishi … niliosema uchaguzi wa marudio ya uchaguzi Zanzibar yanaweza kuviingiza visiwani hivyo kwenye machafuko na umwagaji damu… ni kauli ya raia anayefahamu na hapendezwi na mwenendo wa serikali” alisema Lissu.
Post a Comment