Loading...

Matola, Julio wakosoa tuzo za ligi kuu


matolaaKocha wa zamani wa Simba, Selemani Matola.
Hans Mloli, Dar es Salaam
SIKU chache tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilipotangaza majina ya wanaowania tuzo mbalimbali za Ligi Kuu Bara 2015/16, baadhi ya makocha wazoefu wamekosoa na wengine kusifia kwa wanaowania tuzo hizo zitakazotolewa Julai 17, mwaka huu.
Kocha wa zamani wa Simba, Selemani Matola amepongeza uteuzi wa wanaowania tuzo ya kocha bora kuwa walistahili lakini akakosoa uteuzi wa wanaowania mchezaji bora wa kigeni ambao ni Wazimbabwe, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma wote Yanga na Muivorycoast, Vincent Angban wa Simba.
Wanaopigania tuzo ya kocha bora ni Mholanzi, Hans van Der Pluijm wa Yanga, Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na Salum Mayanga wa Prisons.
jamhuri-kihwelo-julio_7x1b2xzte59i1v7gw0dl3m06bJamhuri Kihwelo ‘Julio’, kocha wa Mwadui FC.
“Kwa makocha naona sawa ila tu wasifanye makosa kama yaliyopita, kama anastahili mgeni wampe mgeni na kama anafaa mzawa basi wampe kwa vigezo kweli, wasipendelee,” alisema Matola na kuongeza:
“Kwa wachezaji wa kigeni naona siyo sawa kuwepo Angban, kuna watu walipaswa kuwepo kama Kipre Tchetche (Azam) au Tambwe (Amissi, Yanga).
“Sijajua wametumia vigezo gani lakini naona Angban hakustahili, Tchetche au Tambwe kila mmoja ameona shughuli yake, walifaa kuwepo sijui kwa nini hawapo.”
Kocha wa zamani wa Yanga, Fred Minziro alisema: “Kwa kocha naona Mzungu (Pluijm) anastahili, timu yake ipo kwenye kiwango kikubwa, imetwaa ubingwa wa ligi, Kombe la FA na bado anaiwakilisha nchi kimataifa.
“Hawa wa kigeni anastahili kupewa Ngoma. Tambwe hayupo lakini naona ni sawa kwa kuwa unaweza kuwa mfungaji bora lakini usiwe kwenye kiwango cha juu, kuna kipindi alipotea kidogo hapa katikati kabla ya kurejea mwishoni mwa ligi.”
Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, kocha wa Mwadui FC naye alisema: “Vyovyote naona sawa maana hizi tuzo huwa wanapanga kwa hisia na si vigezo, mwaka jana walikosea wakampa Makata (Mbwana) na mwaka huu naona vilevile tu.
“Sijisifii lakini kocha bora nastahili kuwa mimi, ukiangalia nimeingia ligi kuu kwa mara ya kwanza, nimemaliza nafasi ya sita, nimekwenda mpaka nusu fainali ya Kombe la FA na yote hayo nimeyafanya bila ya mchezaji wa kigeni hata mmoja, lakini bado tu haitoshi.”
Mbali na tuzo hizo, nyingine 11 zitatolewa siku hiyo ni ya ubingwa wa ligi, makamu bingwa, mshindi wa tatu, mshindi wa nne, timu yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji bora wa ligi, kipa bora, mchezaji bora chipukizi, bao bora la msimu na mwamuzi bora.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright CHACHANDU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top