Taarifa ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) kwa vyombo vya habari leo imeeleza kuwa, Baraza la Eid-El-Fitr kitaifa litafanyia katika Mkoa wa Dar es Salaam,Na kwamba, Swala ya Iddi itaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa moja na nusu asubuhi.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Mohamed Khamis Said, Katibu Mkuu wa Bakwata imeeleza kuwa, sikukuu hiyo inatarajiwa kuwa aterehe 6 au 7 Julai 2016 kulingana na mwandamo wa mwezi.
Pia imeeleza Baraza la Eid El-Fitr litafanyika katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa 10 alasiri.
Post a Comment