Katika hali ya kushangaza siku moja baada ya orodha hiyo kutangazwa, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa wilaya ya Ikungi iliyopo mkoani Singida. Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Bwana Fikiri Avias Said ndani ya masaa 24 tangu uteuzi wake.
Sababu kuu ya Rais kutengua Uteuzi huu ameisema leo hii wakati wa hafla ya kuwaapisha Wakuu wote walioteuliwa, ni kwamba jina lilikosewa, na kusema kwamba Mkuu wa Wilaya halali wa Ikungi ni Bwana Miraji Mtaturu ambaye ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza,
Post a Comment