Loading...

Wengi Hawakumwelewa Lowassa...Kwa Nchi za Kiafrika Kushika Dola Kwa Maandamano ni Kujisumbua Bure

Hakika ni wengi hawakumwelewa lowassa aliposena Chadema iache Mambo ya uharakati ila wajipange kisiasa kushika dola 2020. Ukweli ni kwamba Chadema imetumia fedha nyingi kujitangaza, naona wamefanikiwa kujulikana sana hata kukikosesha amani Chama Tawala ,Sasa ni wakati wa kuweka mikakati ya kuchukua dola. Chadema ina watu wakubwa ndani ya chama ambao wanajua mifumo ya nchi kiusalama.

Ni wakati wao wa kufanya mikakati ya kiakili kushika dola.
Kwa nchi za kiafrika kushika dola kwa maandamano ni kujisumbua bure, cha zaidi mtaishiwa kuuwawa na kuteswa tu

Niwakati wa Ukawa kuwa na timu ya strategy isiyozidi kumi, timu yenye kuaminiana kuhakikisha na wao wanafanya siasa ya kiutu uzima.

Nadhani wakubwa waliopevuka wamenielewaa

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright CHACHANDU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top