Loading...

SHUHUDIA Waziri Mkuu Mstaafu, Sumaye Arejesha Fomu za Uenyekiti CHADEMA

Jana July 14 2016 Waziri mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Frederick Sumaye amerudisha fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kanda ya Pwani, Sumaye ana wapinzani wawili ambao ni John Gugunita na Gango Kidera.

Nafasi zingine za uongozi ambazo zipo wazi ni makamu mwenyekiti ambapo watu watatu wamejitokeza kugombea nafasi hiyo akiwemo Saed Kubenea, nafasi ya mwekahazina wagombea watatu wamejitokeza akiwemo aliyekuwa naibu waziri wa kazi na ajira wa serikali ya awamu ya nne, Makongoro Mahanga.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright CHACHANDU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top