Loading...

Sheikh Ponda Afunguka Kuhusu Fedha Taslimu Zilizotolewa na Magufuli Kwa Ajili ya Hija


Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda hajakubaliana na kitendo cha Rais John Magufuli kutoa fedha taslimu kwa ajili ya kuchangia safari za Hija akisema angezungumza na wahusika ili kujua matatizo ambayo fedha hizo zingesaidia.

Hata hivyo, amempongeza Rais kuahidi kurejesha mali za Waislamu.

Sheikh Ponda, ambaye alipiga simu ofisi za Mwananchi jana asubuhi, amesema ahadi hiyo ya Rais ni ya kuungwa mkono kwa kuwa inaonyesha kujali masilahi ya wananchi, hususan Waislamu.

Juzi, akihutubia Baraza la Idd el Fitr jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema atawasaidia Waislamu kurejesha mali zao na kumpongeza Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Abubakar Zubeir kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kurejesha mali hizo kabla hata hajapewa cheo hicho.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright CHACHANDU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top