Loading...

RAIS Museveni Azua Kihoja..Asimamisha Msafara Wake na Kuketi Barabarani Kupokea Simu

Amini usiamini Rais Yoweri Museveni, alishuka kutoka kwenye gari lake rasmi akachukua kiti chake na kukiweka kando kando ya barabara mpya ya Isingiro ikipitia kijiji hicho cha Kyeirumba hadi Tanzania na kupokea simu faraghani.

Mzee Museveni kama vile baba wa taifa alitumia muda wake kufanya shughuli hiyo huku akiwapungia mkono wapita njia.
Baada ya dakika 30 hivi raia wa kijiji hicho walishangaa kuwa miongoni mwa maafisa wakuu serikalini.

Ilikuwa ajabu sana kwao kumuona Museveni akiwa ameketi barabarani.
Museveni ampandisha cheo mwanaye jeshini

Waganda katika mitandao ya kijamii wamesambaza picha hiyo ya rais museveni akizungumza kwa simu ambayo inaonekana kuwa sio ya kisasa.

Je wewe umewahi kuchukua hatua gani ya kushangaza ili upokee simu ya kibinafsi?

Wengine wanamkejeli kwa kuhofia kudukuliwa huku wengine wakimkosoaa kwa kuketi barabarani.
''Kwani hangeweza kupokea simu yake ndani ya gari lake?"

''Ni siri gani hiyo ambayo hakutaka hata walinzi wake wasikie.

''Ama ilikuwa ni #Besigyexit?", wakizungumzia kuachiliwa kwa dhamana kwa kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye mapema asubuhi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright CHACHANDU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top