MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo imesema kuwa, hoja zilizotolewa na upande wa washtakiwa katika kesi ya uchochezi kwenye Gazeti la MAWIO, hazina mashiko, anandika Faki Sosi.
Washtakiwa kwenye kesi hiyo ni Simon Mkina, Mhariri Mkuu wa MAWIO; Jabir Idrisa, mwandishi mwandamizi wa gazeti hilo; Ismail Mahboob, Meneja wa Kampuni cha Uchapishaji ya Flint na Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki.
Katika mahakama hiyo upande wa utetezi uliiomba mahakama kufuta mashitka yanayowakabili watuhumiwa hao huku upande wa Jamhuri ukitoa hoja za kutaka mashitaka hayo yaendelee kuwepo.
Hoja zilizokuwa zikitolewa na upande wa utetezi zilizowasilishwa na Wakili Peter Kibatala mahakamani hapo ni kwamba, mashitaka matatu yanayowakabili watuhumiwa hao baaada ya kufutwa kwa shitaka namba moja na namba tano, yaliyokuwa yamekosa nguvu kisheria ni pamoja na shitaka namba mbili, namba tatu na namba nne.
Kibatala alidai kuwa, shitaka namba moja la kuchapisha chapisho la uchochozi halina mashiko kisheria kutokana na Katiba ya Tanzania inampa mamlaka Mtanzania kuikosea serikali na kwamba, kilichondikwa hakikuwa uchochezi.
Kibatala alidai kuwa, shitka la kufanya chapisho la uchochezi ambalo lingepelekea hofu kwa Wazanzibar ni kuwa, sheria ya magazeti haitambaui Zanzibar na kwamba, machafuko hayo yangetokea watu hao wasingestahili kushitakiwa mahakamani hapo.
Paul Kadushi, Wakili Mkuu wa Serikali alipinga hoja hizo kwa kudai kuwa, Katiba ya Tanzania na shertia zake inaifahamu kwamba, Tanzania ni pamoja na Zanzibar na kwamba, kosa hilo lilitendwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam na kwamba, watu hao walikuwa sahihi kushitakiwa katika mahakama hiyo.
Thomas Simba, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amesema kuwa, baada ya kusikiliza pande zote mbili na kuzitafrisi kimatakwa ya sheria, ameona kuwa mashitaka hayo yana sababu za kimsingi za kisheria.
Hakimu Simba amesema kuwa, sio kweli kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar ni Tanzania.
Wakati huo huo Robart Katula, mdhamini wa Tundu Lissu aliiambia mahakama hiyo kuwa, mdhana wao hakufika mahakamani hapo kutokana na kuwa mgongwa wa malaria.
Shauri hilio litatajwa tena tarehe 2 Julai kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
Post a Comment